Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/list.ackyshine.com/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Kwa nini vijana wanakatazwa kujamiiana?

Featured Image

Ujana ni kipindi cha mabadiliko kutoka utotoni kuelekea utu uzima, wakati wa kipindi hiki kijana hupata mabadiliko ya kimwili, kiakili na kimtazamo. Mwili na akili hupevuka. Ni kipindi muhimu cha kuweka msingi wa maisha ya baadaye. Vijana wanakatazwa kujamiiana kwa sababu matatizo mengi yanaweza kutokea kutokana na tendo hilo.

Kwanza kabisa kwa kujihusisha na kitendo cha kujamiiana vijana wanapoteza nguvu na muda ambao wangeweza kutumia kwa shughuli za maendeleo. Kwa mfano, kusoma, kufanya kazi, kushiriki katika shughuli za vikundi katika jamii au kucheza michezo.
Pili, matatizo ya mimba katika umri mdogo ni mengi. Mojawapo ni msichana kufukuzwa shule, au hata jamii kumtenga. Matatizo mengine ni ya kiafya kutokana na mwili wa msichana bado kuwa haujakomaa vyema.
Tatu, vijana wanakuwa bado hawajajiandaa kwa uzazi au kujitegemea. Sababu nyingine ya kuwakataza vijana kujamiiana ni ile ya hatari ya kuambukizana magonjwa ya zinaa ikiwa ni pamoja na Virusi vya UKIMWI. Magonjwa haya ni mabaya sana yanaweza kusababisha maumivu makali, ugumba au hata kifo.
Unapofikiria sababu zote hizo utaona kwamba kujamiiana katika umri mdogo kunaweza kuleta madhara mengi kwa afya yako na malengo yako maishani. Hivyo basi unapokatazwa kujamiiana ni kwa sababu ya matatizo haya. Hata hivyo, kama kwa vyovyote huwezi kuacha kujamiiana, hakikisha kwamba unajikinga wewe na mpenzi wako kwa kutumia kondomu.

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, ni tabia zipi zinazochangia kuenea kwa virusi vya UKIMWI?

Je, ni tabia zipi zinazochangia kuenea kwa virusi vya UKIMWI?

Virusi vya UKIMWI kwa kiasi kikubwa vinaenea kwa njia ya kujamii ana. Kama mtu ana wapenzi wengi ... Read More

Je, ni kweli kwamba uvutaji wa bangi hupunguza mawazo?

Je, ni kweli kwamba uvutaji wa bangi hupunguza mawazo?

Bangi hupunguza mawazo kwa muda mfupi kwani huleta hisia za furaha na utulivu. Lakini hata hivyo ... Read More

Dawa za kulevya ni nini?

Dawa za kulevya ni nini?

Tunaposema dawa za kulevya ina maana ni matumizi mabaya ya dawa na hasa pale yatumikapo kinyume c... Read More

Jinsi ya kujikinga na ubakaji

Jinsi ya kujikinga na ubakaji

Hata kama utafanya kila kitu usibakwe bado inaweza ikatokea. Ubakaji na unyanyasaji wa ujinsia unawe... Read More
Je, Ni Sahihi Kutumia Mbinu za Asili za Kuzuia Mimba?

Je, Ni Sahihi Kutumia Mbinu za Asili za Kuzuia Mimba?

Je, ni sahihi kutumia mbinu za asili za kuzuia mimba? Hii ni swali ambalo vijana wengi hujikuta w... Read More

Je, ngono/kufanya mapenzi ni sehemu muhimu ya uhusiano wa kimapenzi?

Je, ngono/kufanya mapenzi ni sehemu muhimu ya uhusiano wa kimapenzi?

Je, ngono/kufanya mapenzi ni sehemu muhimu ya uhusiano wa kimapenzi?

Kwa wengi, kufanya ma... Read More

Vidokezo vya Kukabiliana na Ubaguzi katika Uhusiano wako na Msichana

Vidokezo vya Kukabiliana na Ubaguzi katika Uhusiano wako na Msichana

Ukitafuta vidokezo vya kukabiliana na ubaguzi katika uhusiano wako na msichana, basi umefika maha... Read More

Je, watu wanapendelea ngono/kufanya mapenzi ya kimyakimya au ngono/kufanya mapenzi ya kelele?

Je, watu wanapendelea ngono/kufanya mapenzi ya kimyakimya au ngono/kufanya mapenzi ya kelele?

Je, watu wanapendelea ngono/kufanya mapenzi ya kimyakimya au ngono/kufanya mapenzi ya kelele? Hii... Read More

Je, mwanamke anaweza kufikia mshindo (kufika kileleni)?

Je, mwanamke anaweza kufikia mshindo (kufika kileleni)?

Ndiyo, mwanamke anaweza kufikia mshindo wakati wa kujamiiana. Dalili ya mwanamke kufikia mshindo ... Read More

Je, kwa nini akina mama wajawazito hawatakiwi kunywa pombe?

Je, kwa nini akina mama wajawazito hawatakiwi kunywa pombe?

Wanawake wajawazito ambao hunywa pombe au kuvuta sigara
wanahatarisha afya na maisha ya mtot... Read More

Je, kuna tofauti kati ya mapenzi na ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti kati ya mapenzi na ngono/kufanya mapenzi?

Habari yako rafiki? Natumaini uko salama na unafurahia siku yako. Leo nitazungumzia suala linaloh... Read More

Je, watu wanapendelea kutumia kinga wakati wa kufanya ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanapendelea kutumia kinga wakati wa kufanya ngono/kufanya mapenzi?

  1. Kutumia Kinga Hupunguza Hatari za Maambukizi ya Ngono Kutumia kinga ni hatua muhimu kat... Read More

πŸ“– Explore More Articles
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About