Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/list.ackyshine.com/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Madhara ya dawa za kulevya kwa mwili na ubongo

Featured Image
Moja kati ya vitu vinavyotisha kuhusu dawa za kulevya ni kwamba zinaathiri watu kwa njia mbalimbali na huwezi ukasema kwa uhakika jinsi zitakavyokuathiri. Madhara ya dawa za kulevya yanategemea aina, kiwango na jinsi zitakavyotumika. Vilevile inategemea na umri, afya ya mwili na ukomavu wa akili, na pia mazoea ya matumizi ya dawa hizo. Madhara ya muda hutokea mara tu baada ya dawa za kulevya kutumika, wakati madhara ya muda mrefu huonekana baada ya muda kupita, na mara nyingi husababisha uharibifu wa kudumu kwenye mapafu na ubongo. Kwa mfano, bangi, husababisha kuongezeka kwa mapigo ya moyo, matatizo ya kumbukumbu ya muda mfupi, pamoja na umakini, kujifunza, kufikiri na kutatua matatizo. Pia inaweza ikasababisha kasoro kwenye utaratibu wa viungo vya mwili. Mara kwa mara wavuta bangi huwa na macho mekundu. Na vijana wengine hupata mihemuko mbalimbali kama uoga na hofu baada ya matumizi ya bangi. Dawa za kulevya za vichangamsho, kama mirungi na kokaini, inasemekana kuwa huwafanya watumiaji kuwa macho, kujiona wana nguvu na kujiamini. Vichangamsho vikitumika kwa wingi, humfanya mtumaji kujihisi kuwa na wasiwasi au hofu. Matumizi mabaya ya dawa za kulevya kwa muda mrefu huweza kusababisha matatizo ya akili au hata kifo i iwapo yatatumika kwa kiwango cha juu. Dawa za kulevya zinazokufanya upooze kama heroini au dawa nyingine zinazoagizwa na daktari, husababisha kujisikia umetulia, una amani na furaha. Ukizidisha vipimo husababisha usingizi, upungufu wa umakini na uwezo wa kuona, kizunguzungu, kutapika na kutokwa jasho. Vilevile kipimo kingi kinaweza kusababisha usingizi wa muda mrefu, kuzimia na hata kifo. Pombe za kienyeji kama gongo ni hatari kwa afya na zinaweza kusababisha upofu na hata kifo. Matumizi ya dawa za kulevya hupunguza uwezo wa vijana kuhimili na kutatua matatizo yao ya kijamii na kiakili. Hii husababisha vijana kuwa wepesi kujihusisha na ujambazi na mambo ya ngono na ugomvi, mabadiliko hayo ya tabia husababisha ugomvi katika familia na kuvunjika kwa urafiki. Matumizi ya dawa za kulevya ndiyo sababu kubwa ya ajali za barabarani, kujiua na maambukizo mbalimbali.
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kukabiliana na Hisia za Kufadhaika na Utendaji wa Ngono

Jinsi ya Kukabiliana na Hisia za Kufadhaika na Utendaji wa Ngono

Jinsi ya Kukabiliana na Hisia za Kufadhaika na Utendaji wa Ngono πŸ’†πŸŒ‘οΈ

Karibu kijana... Read More

Vidokezo vya Kuzungumza na Msichana kwa Heshima na Upendo

Vidokezo vya Kuzungumza na Msichana kwa Heshima na Upendo

Kuzungumza na msichana kwa heshima na upendo ni kitu muhimu kwa kila kijana ambaye anataka kuwa n... Read More

Jinsi ya Kuwa na Tarehe ya Ushirikiano na Msichana

Jinsi ya Kuwa na Tarehe ya Ushirikiano na Msichana

  1. Anza kwa Kujijenga Kimaumbile Kabla ya kumwomba msichana tarehe ya ushirikiano, ni muhi... Read More

Magonjwa ya zinaa na dalili zake

Magonjwa ya zinaa na dalili zake

Kuna magonjwa mengi tofauti ya zinaa, lakini yale ambayo yameenea sana ni kisonono, kaswende, klamdi... Read More
Vidokezo vya Kuchagua Tarehe ya Kuvutia na Msichana

Vidokezo vya Kuchagua Tarehe ya Kuvutia na Msichana

Kuchagua tarehe ya kuvutia na msichana inaweza kuwa changamoto sana, lakini kwa bidii na uwezo wa... Read More

Jinsi ya Kuwa na Tarehe ya Kipekee na Ya Kusisimua na Msichana

Jinsi ya Kuwa na Tarehe ya Kipekee na Ya Kusisimua na Msichana

Kila mwanaume anataka kuwa na tarehe ya kipekee na ya kusisimua na msichana. Lakini, wakati mwing... Read More

Je, pombe ni moja ya sababu za kuenea kwa Virusi vya UKIMWI na VVU au magonjwa mengine yatokanayo na kujamiiana?

Je, pombe ni moja ya sababu za kuenea kwa Virusi vya UKIMWI na VVU au magonjwa mengine yatokanayo na kujamiiana?

Matumizi mabaya ya pombe ndiyo yanayosababisha kuenea kwa
VVU au magonjwa mengine yatokanayo... Read More

Ubikira ni nini?

Ubikira ni nini?

Maana halisi ya neno β€œbikira” ni mwanamke au mwanaume ambaye hajawahi kabisa kujamii ana. Kuj... Read More

Je, Ni Lazima Kufanya Ngono Kwa Sababu ya Marafiki au Shinikizo za Kisiasa?

Je, Ni Lazima Kufanya Ngono Kwa Sababu ya Marafiki au Shinikizo za Kisiasa?

Je, ni lazima kufanya ngono kwa sababu ya marafiki au shinikizo za kisiasa? πŸ€”

Ndugu vij... Read More

Njia za Kujenga Hisia za Usalama katika Uhusiano wako na Msichana

Njia za Kujenga Hisia za Usalama katika Uhusiano wako na Msichana

Njia za Kujenga Hisia za Usalama katika Uhusiano wako na Msichana

Hakuna kitu kizuri kama ... Read More

Je, kuna dawa zozote za kutibu magonjwa ya zinaa?

Je, kuna dawa zozote za kutibu magonjwa ya zinaa?

Magonjwa mengi ya zinaa yana dawa za kutibu, kwa mfano: kisonono, kaswende, klamdia, kankroidi au... Read More

ATHARI ZA ULEVI KATIKA JAMII

ATHARI ZA ULEVI KATIKA JAMII

Watu wanokunywa kupitia kiasi huathiri jamii kwa njia mbalimbali. Madhara mengine hutokea kwa kuwa w... Read More
πŸ“– Explore More Articles
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About