Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/list.ackyshine.com/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Jinsi ya kuongeza mvuto kwa mpenzi wako

Featured Image

Kama umeshushwa thamani unakuwa kwenye hatari ya kuachwa. Hata kama mwenzako alikuwa ameshafikiria suala la kuingia kwenye ndoa na wewe lakini kwa sababu ameshakushusha thamani ndoa inaweza kuyeyuka. Ukiwa kwenye ndoa ni hatari zaidi maana mwenzako hukuchukulia wa kawaida mazoea huzidi na hapo ndipo uhitaji wa kuwa na mwingine wa pembeni unapoanzia. Haoni cha muhimu tena kwako, ndiyo maana wazo hilo huvamia ubongo wake kwa kasi sana.

Itafikia hatua, kama upo ndani ya ndoa, mwenzako atagoma kuongozana na wewe na kama ikitokea hivyo mkikutana na rafiki zake njiani hatakutambulisha. Hisia kwamba hamuendani humwingia.

UNAFANYAJE SASA?

Kubwa unalotakiwa kufahamu rafiki yangu mpendwa, suala la kupanda au kushuka thamani lipo mikononi mwako. Yapo mambo ambayo ukiyazingatia, mwenzako hawezi kukuchoka na kufikia hatua ya kukushusha thamani.

Tayari tumeshaona athari zake lakini hapa sasa nataka kukupa mbinu ambazo ukiwa nazo makini basi itakuwa rahisi kwako kubaki namba moja na mtu muhimu zaidi (ndiyo inavyotakiwa kuwa) kwa mpenzi wako maana ni haki yako.

ANZIA MWANZO

Ni rahisi zaidi kulinda thamani yako kuanzia mwanzo wa uhusiano wenu. Ikiwa tayari mmeshakomaa halafu tatizo hilo likajitokeza, hutumika nguvu nyingi zaidi kulirekebisha kuliko kujizatiti kuanzia mwanzo wa uhusiano. Ni mambo gani hayo? Twende hapo chini.

CHUNGA KAULI ZAKO

Naomba ieleweke wazi kuwa mada hii ni maalum zaidi kwa wanawake. Kitu muhimu cha kwanza kabisa kwa mwanamke ambaye anataka kuilinda thamani yake kwa mpenziwe ni kupima sana kauli zake.

Acha kuropoka hovyo, pima maneno yako na ikiwezekana kama unadhani kuna jambo huna uhakika nalo usizungumze kabisa. Katika eneo hili, uwe makini zaidi mnapokuwa na watu wengine. Kama mwanamke usiwe mchangiaji hoja sana.

Utulivu wako unaweza kuwa silaha kubwa ya kukufanya ubaki na thamani yako kama mwanamke anayejitambua.

USIRUHUSU MAPENZI

Msichana mwenye kujitambua na kufahamu thamani yake sawasawa hawezi kuruhusu mwili wake ujulikane na mwanaume harakaharaka. Onesha unajitambua na usikubali kirahisi kuuacha mwili wako uchezewe.

Mpe hoja; kwanza mapema, hajakuoa wala kukuchumbia, haraka ya nini? Wakati unawaza kuhusu kutoa penzi lako, lazima ufikirie kuhusu athari zinazoweza kukupata kwa kukurupukia mapenzi. Mwanaume ambaye bado hamjachunguzana na huna uhakika naye wa kutengeneza maisha, kichwani mwake hakuweki kwa asilimia kubwa.

Ukumbuke kwamba, ukipata matatizo yoyote – binafsi au yanayosababishwa na uhusiano wenu, anakuwa hana uwajibikaji wa asilimia kubwa kwa tatizo hilo. Utabaki wewe na matatizo yako!

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE
[products columns="2" ids="30827"]
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Kuunda Mipango ya Burudani na Shughuli za Familia katika Familia Yako

Kuunda Mipango ya Burudani na Shughuli za Familia katika Familia Yako

Kuunda mipango ya burudani na shughuli za familia katika familia yako ni muhimu sana. Inasaidia k... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Kujifunza na Kuendeleza Maarifa katika Familia

Kuweka Kipaumbele cha Kujifunza na Kuendeleza Maarifa katika Familia

Kuweka kipaumbele cha kujifunza na kuendeleza maarifa katika familia ni jambo muhimu sana katika ... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha urafiki na jamaa

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha urafiki na jamaa

Mahusiano ya kimapenzi na ya kijamii ni muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku. Lakini, inak... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha urafiki na watu wenye ulemavu

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha urafiki na watu wenye ulemavu

  1. Tafuta shughuli ambazo zinawezekana kwa wote wawili. Mara nyingi, watu wenye ulemavu wa... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Uvumilivu na Mshikamano katika Familia

Kuweka Kipaumbele cha Uvumilivu na Mshikamano katika Familia

Kuweka Kipaumbele cha Uvumilivu na Mshikamano katika Familia

Familia ni muhimu sana katika... Read More

Kuhamasisha Kujitambua na Kujielewa katika Mahusiano

Kuhamasisha Kujitambua na Kujielewa katika Mahusiano

  1. Kujitambua na Kujielewa ni jambo muhimu sana katika mahusiano. Kujitambua kunamaanisha ... Read More

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Ushirikiano katika Familia: Kuhamasisha Ushirikiano wa Timu

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Ushirikiano katika Familia: Kuhamasisha Ushirikiano wa Timu

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Ushirikiano katika Familia: Kuhamasisha Ushirikiano wa Timu

<... Read More
Kukabiliana na Mabadiliko ya Kimwili katika Kufanya Mapenzi: Jinsi ya Kuheshimu na Kukubali

Kukabiliana na Mabadiliko ya Kimwili katika Kufanya Mapenzi: Jinsi ya Kuheshimu na Kukubali

Kukabiliana na Mabadiliko ya Kimwili katika Kufanya Mapenzi: Jinsi ya Kuheshimu na Kukubali

<... Read More
Mambo 10 ambayo wanawake wamewazidi wanaume

Mambo 10 ambayo wanawake wamewazidi wanaume

1. Wana Nguo Nyingi KulikoWanaume.
2. Wanafahamu Nani Ni Baba HalisiWa Watoto Wao.

3. N... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya ujasusi na ulinzi wa taifa

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya ujasusi na ulinzi wa taifa

Mapenzi ni muhimu sana katika maisha yetu na yanatakiwa kulindwa kwa kila hali. Hata hivyo, kuna ... Read More

Kutumia Vifaa vya Kufanya Mapenzi: Kuingiza Burudani katika Uhusiano wako

Kutumia Vifaa vya Kufanya Mapenzi: Kuingiza Burudani katika Uhusiano wako

  1. Kuweka Burudani katika Uhusiano wako

Uhusiano wa kimapenzi unaweza kuhitaji u... Read More

Jinsi ya Kuwa Msaada katika Safari ya Kiroho ya mke wako

Jinsi ya Kuwa Msaada katika Safari ya Kiroho ya mke wako

Kuwa msaada katika safari ya kiroho ya mke wako ni jambo muhimu katika kujenga uhusiano wa kiroho na... Read More
πŸ“– Explore More Articles
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About