Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/list.ackyshine.com/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua: Funzo kwa mabinti

Featured Image

Kijana maskini na mwenye maisha duni alimpenda msichana mmoja
Baada ya kutumia muda mwingi kumfikiria msichana huyo,
Siku moja akaamua kumwita na kumwambia ukweli ya kwamba amempenda na angehitaji kumuoa.

Msichana kwa nyodo na jeuri akasema "sikiliza tena unisikilize kwa makini wewe maskini mshahara wako unaopokea kwa mwezi hautoshi hata kwa matumizi yangu ya siku moja sasa utawezaje kunitunza mm!

Kwaufupi mm sio levo zako hivyo basi sahau kabisa kuhusu kunipata mimi
Nenda katafute maskini mwenzio atakae endana na maisha yako,
Mwisho akamwangalia kwa dharau na kisha akaenda zake.

Kwanzia siku ile kijana hakubahatika tena kumuona msichana yule lkn kwakuwa alimpenda basi hakuweza kumsahau kirahisi rahisi siku zilienda na miezi ikasonga,
Miaka 10 baadae wawili hawa walikuja kukutana katika supermarket moja hivi mjini

Kijana alipomwona msichana alitabasamu lakin kabla hajasema chochote msichana kama kawaida yake kwa dharau akasema "we maskin upo! hivi na ww unaingiaga supermarket eh!

Akaongeza huku akisema walau sasahivi nakuona umependeza inaonekana boss wako kakuongeza mshahara
ila kwa kifupi naomba nikwambie sasahivi nimeshaolewa mume wangu anafanya kazi kwenye kampuni moja hivi ya mtu binafsi kampuni maarufu sana na mshahara wa mume wangu ni shilingi milioni moja na laki mbili kwa mwezi na malupulupu mengine kibao,
Unafikiri ww na umaskini wako kuna siku utakuja kufikia kiwango cha mshahara anachopokea mume wangu!

Macho ya kijana yalitokwa na machozi kwa kuona msichana hajabadilika na anaendelea kuwa na maneno ya kejeri na dharau.

Mara hii mume wa yule dada akaingia ktk supermarket
Ile kumuona yule kijana mume akasema "ooh! Kiongozi upo hapa! Leo imekuwa bahati umekutana na mke wangu!" Kisha akamgeukia mke wake na kusema "mke wangu huyu ndo boss wangu

Na unajua nn mke wangu usishangae kumuona boss wangu anakuja kununua vitu mwenyewe hapa supermarket ukweli ni kwamba boss wangu hana mke, anasema alisha wahi kumpenda msichana mmoja lakini hakufanikiwa kumpata na amekuwa na ndoto ya kuja kukutana tena na msichana huyo ndio maana mpaka sasa bado hajaoa.

Akaendelea kusema hebu fikiria ni bahati kiasi gani alikuwa nayo msichana huyo kama angekubali kuolewa na boss wangu leo hii siangekuwa
maisha!

Muda wote msichana alikuwa kimya hajui hata ajibu nn kwa dharau alizomuonyesha kijana tangu mwanzo.

UJUMBE WANGU
Kwenye maisha mambo huweza kubadilika kama vile upepo unavoweza kubadili mwelekeo kulingana na masaa Hivyo basi usimdharau na kumbeza mtu yeyote kwa sababu ya hali aliyonayo,
Maana kila mtu anafungu lake alilopangiwa na Mungu,

Lakini pia kumbuka hakuna ajuaye kesho
Wakati mwingine mtu unayemdharau leo ndiye huyohuyo ambaye kesho utasimulia mafanikio yake.

Kwako unayesoma ujumbe huu nakuombea Mungu akakufungulie milango ya baraka na kuyapa thamani maisha yako ili pale ulipozomewa ukashangiliwe na wale wote waliokudharau punde wakapate kukupigia magoti kwa uweza wa Mungu.

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

Director J (User) on May 15, 2025

Good story πŸ’ͺ

Related Posts

Jinsi ya Kujitolea kwa Upendo katika Familia: Kuwasaidia Wengine kwa Furaha

Jinsi ya Kujitolea kwa Upendo katika Familia: Kuwasaidia Wengine kwa Furaha

Leo tutaangalia jinsi ya kujitolea kwa upendo katika familia na kuwasaidia wengine kwa furaha. Fa... Read More

Jinsi ya Kudumisha Heshima na Utu katika Familia: Kuheshimu Tofauti na Upekee

Jinsi ya Kudumisha Heshima na Utu katika Familia: Kuheshimu Tofauti na Upekee

Familia ni sehemu muhimu sana katika maisha yetu. Ni mahali ambapo tunakua na kujifunza maadili y... Read More

Jinsi ya Kujenga Mazoea ya Kupenda na Kuheshimu katika Familia

Jinsi ya Kujenga Mazoea ya Kupenda na Kuheshimu katika Familia

Kujenga mazoea ya kupenda na kuheshimu katika familia ni muhimu sana kwa afya na ustawi wa famili... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Kusamehe na Kupokea Upendo katika Familia Yako

Kuweka Kipaumbele cha Kusamehe na Kupokea Upendo katika Familia Yako

Kuweka Kipaumbele cha Kusamehe na Kupokea Upendo katika Familia Yako

Familia ni kitu cha t... Read More

Kuunda Uhusiano wenye Furaha na Chanya na Marafiki wa Mwenzi wako

Kuunda Uhusiano wenye Furaha na Chanya na Marafiki wa Mwenzi wako

Kuunda uhusiano wenye furaha na chanya na marafiki wa mwenzi wako ni muhimu sana katika kudumisha... Read More

Kufurahia Kujamiiana kwa Kujielewa: Kuhamasisha Utambuzi wa Kijinsia na Uhuru

Kufurahia Kujamiiana kwa Kujielewa: Kuhamasisha Utambuzi wa Kijinsia na Uhuru

Kufurahia Kujamiiana kwa Kujielewa: Kuhamasisha Utambuzi wa Kijinsia na Uhuru

Ni muhimu sa... Read More

Jinsi ya kusuluhisha Migogoro mke wako

Jinsi ya kusuluhisha Migogoro mke wako

1. Kuwa na Mawasiliano Mzuri: Anza kwa kuwa na mawasiliano mazuri na mke wako. Jenga mazingira ya wa... Read More
Kujenga Ushirikiano wa Karibu na Wazazi na Familia katika Mahusiano

Kujenga Ushirikiano wa Karibu na Wazazi na Familia katika Mahusiano

  1. Kuwa wazi na Wazazi na Familia Kujenga ushirikiano wa karibu na wazazi na familia ni mu... Read More

Kukabiliana na Mazoea ya Kutokuwa na Ushirikiano na Kutoelewana katika Familia Yako

Kukabiliana na Mazoea ya Kutokuwa na Ushirikiano na Kutoelewana katika Familia Yako

  1. Kukabiliana na Mazoea ya Kutokuwa na Ushirikiano na Kutoelewana katika Familia Yako
  2. Read More
Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kiswahili na lugha nyingine na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kiswahili na lugha nyingine na mpenzi wako

Katika mapenzi, kuelewa tofauti za lugha ni muhimu sana. Ikiwa wewe na mpenzi wako mnazungumza lu... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Ubora wa Mahusiano: Jinsi ya Kutunza Ushirikiano wako

Kuweka Kipaumbele cha Ubora wa Mahusiano: Jinsi ya Kutunza Ushirikiano wako

Kuweka Kipaumbele cha Ubora wa Mahusiano: Jinsi ya Kutunza Ushirikiano wako

Mahusiano ni s... Read More

Njia za Kupunguza Mazoea ya Ubaguzi katika Mahusiano: Kujenga Usawa na Ushirikiano

Njia za Kupunguza Mazoea ya Ubaguzi katika Mahusiano: Kujenga Usawa na Ushirikiano

Mahusiano yoyote yanahitaji usawa na ushirikiano kati ya wapenzi. Hata hivyo, wakati mwingine huw... Read More

πŸ“– Explore More Articles
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About