Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/list.ackyshine.com/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua cha kijana na mke wake na mama yake

Featured Image

Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa. Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwambia chagua mawili imma kunioa mimi au kukaa na mama yako, kwa sababu ukinioa mimi sitokubali mama yako aje hata harusini kwangu! Yule kijana aliemewa. Hakujua la kufanya. Mke anamtaka, lakini mama yake pia anampenda.

Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu. Alimwambia: moyo wangu unampenda mno binti niliyekwenda kumposa, lakini pia siwezi kuishi mbali na mama yangu. Nifanye nini?

Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa kijana yule, alimjibu kwa kumwambia: Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao, rudi nyumbani, na leo usifanye chochote, ila kuikosha mikono ya mama yako. Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake. Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya ajizi yoyote.

Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa kwa kazi za sulubu, alilia sana. Muda wote huu alikuwa hajawahi kuangalia viganja vya mama yake. *Je, na wewe umewahi kukaa na kuangalia viganja vya mama au baba yako kuona tabu walizopitia kukulea?* Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kusamehe kila kitu kwa ajili ya mustakbali wa mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, kukosha nguo, kupiga deki na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea chumo la halali bila ya kujali ugumu wa jkazu hiyo.

Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana mustakbali mzuri. Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia, siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya mtu asiyejua thamani ya mama. Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi! Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya leo yangu wakati yeye ameuza maisha yake yote kwa ajili ya mustakbali wangu.
NANI KAMA MAMA?!? Maa! Tabasamu lako ni ufunguo wangu wa ofanisi.
Kama umeipenda.

Share kwa wengine ili nao wazinduke.

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE
[products columns="2" ids="30827"]
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Kuweka Kipaumbele cha Muda wa Kufurahisha Pamoja na Familia Yako

Kuweka Kipaumbele cha Muda wa Kufurahisha Pamoja na Familia Yako

Kuweka kipaumbele cha muda wa kufurahisha pamoja na familia yako ni muhimu sana kwa afya na furah... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya mila na tamaduni za familia zenu

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya mila na tamaduni za familia zenu

Leo hii, nataka kuzungumzia kuhusu jinsi ya kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya mila na ... Read More

Jinsi ya Kujenga Ushirikiano wenye Furaha na Mafanikio katika Familia Yako

Jinsi ya Kujenga Ushirikiano wenye Furaha na Mafanikio katika Familia Yako

Kujenga ushirikiano mzuri na wa furaha na mafanikio katika familia yako ni muhimu sana kwa ustawi... Read More

Msaada na Ushirikiano katika Familia: Kuweka Wanafamilia Kwanza

Msaada na Ushirikiano katika Familia: Kuweka Wanafamilia Kwanza

  1. Msaada na Ushirikiano Katika Familia Ni Muhimu Sana

Katika jamii yetu, famili... Read More

Je, ni njia gani zinaweza kuleta hisia za kihisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, ni njia gani zinaweza kuleta hisia za kihisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, ni njia gani zinaweza kuleta hisia za kihisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi? Swali hili lin... Read More

Jinsi ya Kukuza Kujithamini katika Familia: Kuimarisha Nguvu ya Kujiamini

Jinsi ya Kukuza Kujithamini katika Familia: Kuimarisha Nguvu ya Kujiamini

  1. Tambua Thamani yako kama Mtu: Kujithamini ni muhimu sana katika familia, kwa sababu una... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu uzazi na mipango ya familia

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu uzazi na mipango ya familia

Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu uzazi na mipango ya familia ni mchakato muhimu katika uhusiano wen... Read More
Njia za Kupunguza Mazoea ya Kukosa Ushirikiano na Kuunda Amani na Furaha katika Familia

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kukosa Ushirikiano na Kuunda Amani na Furaha katika Familia

  1. Kuwasiliana kwa Ukaribu: Katika familia, kuna umuhimu wa kuzungumza na kuwasiliana kwa ... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Kujenga Ushirikiano wa Kiroho katika Familia

Kuweka Kipaumbele cha Kujenga Ushirikiano wa Kiroho katika Familia

Kuweka Kipaumbele cha Kujenga Ushirikiano wa Kiroho katika Familia

  1. Kujenga ushir... Read More

Jinsi ya Kuelewa na Kujibu Mahitaji ya Mapenzi ya mke wako

Jinsi ya Kuelewa na Kujibu Mahitaji ya Mapenzi ya mke wako

Kuelewa na kujibu mahitaji ya mapenzi ya mke wako ni muhimu katika kudumisha uhusiano wa karibu na w... Read More
Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Heshima katika Mahusiano: Kuweka Mipaka na Kuheshimiana

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Heshima katika Mahusiano: Kuweka Mipaka na Kuheshimiana

Habari za leo wapenzi wa Kiswahili! Leo tutajadili kuhusu kukabiliana na mazoea ya kukosa heshima... Read More

Jinsi ya Kutunza Afya yako Mwenyewe wewe kama Mwanamme

Jinsi ya Kutunza Afya yako Mwenyewe wewe kama Mwanamme

Read More
πŸ“– Explore More Articles
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About