Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/list.ackyshine.com/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE 🔁
AckyShine

Namna nzuri ya kuhudumia nywele zako za asili kirahisi

Featured Image
Kwa wale ambao tuna nywele asilia (natural hair), tayari tunafahamu changamoto kadhaa tunazokumbana nazo. Kwa wale mnaofikiria kuanza kuwa na nywele asilia, karibuni sana tuendelee kujuzana namna ya kutunza nywele zetu kama tulivyopewa na Mungu. Katika mada ya leo, nitakwenda kuzungumzia vitu vya kuzingatia ili kuikuza nywele yako asilia kwa haraka zaidi. Je,unazifahamu nywele zako vizuri?Una nywele za aina gani? Zina tabia gani? Zinataka nini? Zifuatazo ndizo njia ya kuzihudumia nywele zako;

1. Kuzikubali kama zilivyo na kuzipenda.

Utasikia ..hiki kipilipili changu ni steelwire ya kimataifa, ..hakitikisiki hata upepo wa dunia yote ungevumia pande hizi. Mwingine oh..nywele zangu kama miti ya mibuyu kichwani…hazishikiki.T atizo ni kwamba hamjafahamiana vizuri yani wewe na nywele zako. Hata mimi niligombana nazo sana huko nyuma kabla ya kuzielewa vizuri. Jenga mahusiano mazuri tu na nywele zako,zielewe,ukifikia hapo utaanza kuzipatia hata hazitakusumbua.

2. Usafi wa ngozi ya nywele na nywele zenyewe.

Nywele zenye afya huanzia kwenye ngozi safi ya nywele.Nafahamu unataka nywele zako zisidumae kwa hiyo zioshe vizuri.Wakati uliopita nilizungumzia kuziosha kwa product zilizo rafiki( ‘friendly’) .Ngozi safi ya nywele itasababisha nywele kupata njia ya kujitokeza nje kwa urahisi.Unapoziacha chafu,ule uchafu unaziba matundu ya nywele zako na kuzuia njia,kama ambavyo matundu ya uso yakiziba unapata machunusi maana uchafu unajaa basi kwa nywele hazitakua vizuri.

3. Linda unyevu wa nywele zako

Kila mtu akisikia kiu hunywa maji.Nywele zako zinahitaji kulindwa zisisikie kiu.Unapoziosha,yale mafuta asilia ya kuzilinda huondoka na uchafu.Nywele inabaki ikiwa na udhaifu fulani maana haiwezi hata kushikilia hayo maji yaliyopo vizuri,na zikikauka zinakua kavu sana.Ni vizuri kabla hazijakauka vizuri,ukazi-’condition’.Kwa nywele ambazo ni nyepesi na chache,pia kuna product za kuzisaidia ziweze kutunza vizuri unyevu na hivyo kuwa na afya nzuri.

4. Zifahamu nywele zako

Yani hapa ndo shule ilipolalia kabisaa maana ukizijua tu basi utazihudumia kwa usahihi. Unatakiwa kuangalia namna gani nywele zako zinanyonya unyevu .Unajuaje? Chukua kikombe,kijaze maji safi.Ukipata glass itakuwa vizuri zaidi. Chomoa unywele mmoja kichwani,hakikisha unatoka na kale kamzizi kake keupe keupe hivi. Tumbukiza unywele wako kwenye glass yako ya maji hakikisha imeingia yote.Kama ikizama hapo hapo na hainyanyuki tena,basi nywele zako zinanyonya unyevu kwa haraka kabisa.Kama inachukua muda kuzama,au haizami kabisa,nywele zako zinanyonya unyevu taratibu au zinanyonya kwa shida. (Wala usihofu,zipo namna ya kuzifanya zinyonye unyevu kwa haraka,tutajuzana.)Ni kwamba ‘cuticle’ zake zimefunga haswa,ndio maana unyevu au maji haviingii kwa haraka. Kwa hiyo ukifanya ‘deep conditioner’ kwa kutumia joto kama la drier lakini uwe moto mdogo sana au ufanye ‘hot oil treatment’ itakusaidia ‘cuticle’kufunguka na unyevu kupita. Mbadala,unaweza baada ya kuosha suuza na maji ya vuguvugu halafu weka mafuta ya kimiminika.Inasaidia sana. Mimi nina aina gani?..Nina nywele zinazonyonya unyevu haraka.

5. Mafuta ya Kupaka kichwani.

Ni ya muhimu mnoo!.Nimefanya utafiti wa kina nimeona mafuta ya nazi yanaweka afya nzuri kwa nywele aina nyingi hivyo na mimi nikaanza kuyatumia. Kwangu mimi,mafuta ya nazi ya kutengeneza mwenyewe yamenikubali sana. Japo huwa nanunua pia mafuta kama ya olive(extra virgin) na ya tea tree.

6. Kuzichambua vizuri kabla ya kuchana.

Uwe mkarimu na mwenye subira kwa nywele zako. Mimi zikijifunga huwa nazichambua kwa mikono taratibu wakati mwingine nazilowesha na maji kwa mbali halafu nachana kwa chanuo lenye mapana sio ambalo reli zake zimebanana. sio kitana. Chanuo kubwa(wide toothed comb).

7. Usizisumbue mara kwa mara na usuke mitindo ya kuzitunza zikue.

Kama unataka zikue haraka, usizisumbue sana. Unaweza ukasuka mitindo mizuri tu ukakaa nazo wiki nzima au kadri zitakavyodumu. Au upunguze kuzichana mara kwa mara lakini utafute siku kama wikiendi ukae uzichambue taratibu na vidole kuondoa mafundo. Kuchana mara kwa mara zinapukutika,zinaanguka. Zitakua lakini sio kwa kasi ya kama ukizisuka ukaziacha kwa muda.

8. Punguza matumizi ya vitu vya moto kwenye nywele zako kama pasi ya nywele na vingine vya hivyo.

Mimi dryer la nywele situmii zaidi ya mara mbili kwa mwezi. Mara nyingi naziacha zikauke na hewa hata kama nimezifunga rollers natoa kesho baada ya masaa 24
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Mavazi ya Ofisini kwa Wadada

Mavazi ya Ofisini kwa Wadada

Wengi wetu tunashindwa kutofautisha mavazi ya sehemu husika mfano Ofisini, michezoni, na yale ya ... Read More

Mambo ya msingi kwa mwanamke kuyajua unapojiremba

Mambo ya msingi kwa mwanamke kuyajua unapojiremba

Kope nazo humpendezesha mwanamke kuna aina ya rangi za kupaka kwenye kope, lakini zinatofautiana. Ni... Read More
Jinsi ya kusafisha na Kutunza Kucha zako

Jinsi ya kusafisha na Kutunza Kucha zako

Inashauriwa kwamba kabla ya kuchukuwa uamuzi wa kwenda kununua vifaa husika ambavyo utavitumia un... Read More

Jinsi ya Kujaza nywele kwa njia za Asili

Jinsi ya Kujaza nywele kwa njia za Asili

Zingatia mambo haya yafuatayo;

  1. Chukua parachichi kubwa moja, asali vijiko vitatu na ki... Read More
Uvaaji wa Tai na Maana yake

Uvaaji wa Tai na Maana yake

Wachambuzi wa mambo ya saikolojia wanasema kwamba kwa kuchukua tai na kulivaa ile rangi ndiyo ita... Read More

Jinsi ya kuchagua rangi sahihi wakati wa Kujipodoa

Jinsi ya kuchagua rangi sahihi wakati wa Kujipodoa

YAPO mambo mabalimbali katika tasnia ya urembo hasa katika vipodozi yanayopaswa kuzingatiwa katik... Read More

Jinsi ya kuvaa viatu mbalimbali inavyotakiwa na ili upendeze

Jinsi ya kuvaa viatu mbalimbali inavyotakiwa na ili upendeze

Viatu ni kinga kwa ajili ya kuhifadhi miguu. Vile vile viatu ni vazi ambalo linaongeza urembo na ... Read More

Jinsi ya Kujiremba Macho

Jinsi ya Kujiremba Macho

Kuna urembo mbalimbali wa macho kulingana na taste ya mtu na mapendeleo yake . Leo nitazungumzia ... Read More

Faida za kuogea maji ya Moto

Faida za kuogea maji ya Moto

Watu wengi hupendelea kutumia maji ya moto kuoga pale hali ya hewa inapobadilika na kuwa ya barid... Read More

Jinsi ya kuondoa kitambi Kitaalamu

Jinsi ya kuondoa kitambi Kitaalamu

Hapo zamani kidogo tuliona na tulishuhudia watu wakisema ya kwamba mwanaume ambaye ana kitambi nd... Read More

Madhara ya kuchora tattoo mwilini

Madhara ya kuchora tattoo mwilini

Tattoo ni nini?
Hii ni uwekaji wa wino kwenye ngozi ya ndani kitaalamu kama... Read More

Namna ya Kuifanya ngozi yako kuwa laini bila Madoa

Namna ya Kuifanya ngozi yako kuwa laini bila Madoa

Ili kufanya ngozi yako kuwa laini bila madoa zingatia mambo haya yafuatayo;

1.TUMIA ANTIOX... Read More

📖 Explore More Articles
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About