Nikitafuta rafiki kwa nia ya kuoana (mchumba), je ni sifa gani niangalie kwa msichana/mvulana?
Date: April 17, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Kuchagua mchumba ni moja ya maamuzi ambayo kijana anahitaji kuyafanya kwa uangalifu mkubwa sana. Kwa sababu huyo ndiye atakayekuwa mwenzi wake wa maisha. Katika kuchagua mchumba kila mtu ana mawazo yake kuhusiana na kilicho muhimu kuzingatiwa. Mara nyingi mhemuko una nguvu zaidi kuliko uamuzi wa kimantiki
Hata hivyo, vifuatavyo ni kati ya vigezo ambavyo vinaweza kuangaliwa:
β’ Chagua mtu anayekuheshimu wewe na wengine; Chagua mtu unayemwamini;
β’ Chagua mtu ambaye unaweza kuongea, kujadiliana, na kuhojiana naye kwa uwazi bila kugombana;
β’ Chagua mtu mwenye umri unaokaribiana na wa kwako;
β’ Chagua mtu anayependelea vile unavyopendelea;
β’ Chagua mtu ambaye ataelewa matatizo yako na yuko tayari kukusaidia kuyatatua; na
β’ Chagua mtu mwenye afya nzuri.
Hii inamaanisha pia kumpata mtu ambaye kabla ya kuanza kujaamiana naye, atakuwa tayari kwenda kupima kwa hiari kujua hali yake ya VVU na pia kuwa tayari kutumia kinga kwa maana ya kondomu hadi hapo mtakapojua hali zenu.
Wafahamishe wazazi wako mtu uliyemchagua kama mchumba na mtambulishe kwao i ili wamfahamu na yeye awafahamu wazazi wako. Wakati huohuo na wewe jaribu kuwafahamu wazazi wake. Usifanye uchumba wa haraka. Pata muda wa kutosha kumwelewa rafiki yako.
Please log in or register to leave a comment or reply.
Related Posts
Je, ni muhimu kujadili mipaka na dhibitisho wakati wa ngono/kufanya mapenzi? Ndio, ni muhimu sana...
Read More
Vidonge na sindano zinazuia mimba kwa kuzuia yai lisipevuke. Akitumia njia hizi za kuzuia mimba, ...
Read More
Tunatofautisha dawa za kulevya katika makundi mawili. Zile zinazokubalika na zile zisizokubalika ...
Read More
Ni kweli kwamba wakati wa kujamii ana na kutunga mimba ni mbegu moja tu ya kiume i inayopenya kwe...
Read More
Unywaji wa pombe ni sehemu ya utamaduni wa Tanzania na nchi
nyinginezo duniani.
Watu h...
Read More
Leo tutaongelea kuhusu umuhimu wa kujadili mipaka ya faragha katika uhusiano wa ngono au kufanya ...
Read More
-
Kujenga uhusiano wa kimapenzi wenye afya na mwenza wako ni muhimu sana. Hii ni kwa saba...
Read More
Hii ni kweli kabisa. Watu wanaoishi na ualbino ni watu wa
kawaida kama binadamu wengine wote...
Read More
Jinsi ya Kutambua Ishara za Kuwa Tayari kwa Ngono π
Karibu kijana, leo tutaongelea jamb...
Read More
Ndiyo, mtu yoyote anayelazimishwa
kujamiina atakuwa
amebakwa, haijalishi kama
mtu ...
Read More
Upendo ni hisia ambazo zinafanya maisha kuwa na maana zaidi. Kila mtu anapaswa kupata upendo, na ...
Read More
Sheria ya Tanzania inaeleza dawa zilizo halali na zisizo halali.
Tumbaku imekubalika na jami...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!