Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/list.ackyshine.com/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Njia za Kuzuia Mimba

Featured Image
Njia za uzazi wa mpango zinatofautiana sana na zinaweza kugawanywa katika makundi mengi:

Vizuizi

(hizi huzuia mbegu kulifikia yai): Kuna mpira wa kiume (kondomu ya kiume), yaani mfuko wa mpira uliozibwa upande moja. Unavishwa kwenye uume uliosimama kabla ya kuingia ukeni. Pia kuna mpira wa kike (kondomu ya kike), yaani mpira unaoingizwa ukeni kabla ya kujamiiana.

Vidonge vya kuzuia mimba:

Lazima mwanamke anywe vidonge hivi kila siku hata kama hajamiiani.

Njia nyingine za kuzuia mimba kwa muda mrefu

. Njia hizi hazihitaji maandalizi maalum, ili kuzuia mimba, kabla ya kujamiiana na pia mwanamke hahitaji kukumbuka kufanya chochote kila siku. Kati ya njia hizi ni pamoja na sindano anazopewa mwanamke kila baada ya miezi mitatu. Pili, kuna vipandikizi, yaani vijiti vyembamba vya plastiki vinavyowekwa kwenye sehemu ya juu ya mkono wa mama kwa njia ya upasuaji mdogo. Vijiti vina kichocheo kinachozuia kupevuka kwa yai. Pia, kuna kitanzi ambacho ni kitu kidogo kilichotengenezwa kwa aina maalum ya plastiki. Kwa ufupi kinaitwa IUD. Huwekwa kwa utaalamu ndani ya mfuko wa uzazi. Sindano, vipandikizi na vitanzi lazima viwekwe na mtaalamu mwenye ujuzi kwenye kituo cha afya chenye vifaa vya kutosha. Kwa vile dawa za kuzuia mimba kwa muda mrefu zinaingiliana na mzunguko wa kawaida wa hedhi kwa kiasi, athari zake ni kubwa kuliko kutumia vidonge.

Kwa mwanaume na mwanamke kuna njia ya kudumu ya kufunga kizazi kwa njia ya upasuaji

. Kwa mwanaume mirija inayopitisha mbegu hukatwa na kufungwa, ili kuzuia mbegu zisitoke. Akijamiiana, anaweza kumwaga shahawa, lakini ndani ya shahawa hakuna mbegu. Kama mwanaume amefunga kizazi uume utadinda kama kawaida na kufikia mshindo atamwaga maji ya shahawa ambayo hayatakuwa na mbegu. Kwa mwanamke mirija ya kupitisha mayai hukatwa na kufungwa, ili kuzuia mayai kufika kwenye mfuko wa uzazi. Baada ya upasuaji huu, mama ataendelea na hedhi kama mwanzo, lakini yai halitaweza kukutana na mbegu za kiume tena. Vilevile kuna njia nyingine mbalimbali ambazo hazina uhusiano na matumizi ya dawa au vizuizi vya mimba. Njia hizi hazina uhakika mkubwa wa kutopata mimba. Mara nyingine mama anatumia ishara mbalimbali, au tarehe kujua lini anaweza kupata mimba, ili kuepuka kujamiiana katika kipindi hicho. Kumwaga mbegu za kiume nje ya uke, au kutegemea kwamba mimba hazishiki wakati wa kunyonyesha ni njia nyingine za asili zinazotumiwa. Kumbuka kwamba njia hizi hutumika sana, lakini si njia salama sana za kuzuia mimba wala kuambukizwa na magonjwa ya zinaa. Ni muhimu kukumbuka kwamba njia ya uzazi wa mpango inaweza kufaa kwa mtu huyu na isifae kwa mtu mwingine. Kwa hiyo, ni vizuri kila mtu aliyeamua kupanga uzazi apate ushauri kwenye kliniki kuhusu njia inayomfaa zaidi
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Nifanyeje Kuelewa umuhimu wa Kujikinga na Maambukizi ya UKIMWI?

Nifanyeje Kuelewa umuhimu wa Kujikinga na Maambukizi ya UKIMWI?

Nifanyeje Kuelewa Umuhimu wa Kujikinga na Maambukizi ya UKIMWI? 🌍

Leo, tutaangazia umuh... Read More

Je, baada ya kutumia vidonge au sindano kwa muda mrefu, mwamamke akiacha kuzitumia hizo njia ataweza kupata mimba tena?

Je, baada ya kutumia vidonge au sindano kwa muda mrefu, mwamamke akiacha kuzitumia hizo njia ataweza kupata mimba tena?

Vidonge na sindano zinazuia mimba kwa kuzuia yai lisipevuke. Akitumia njia hizi za kuzuia mimba, ... Read More

Nifanyeje Kukabiliana na Hisia za Kukosa Ujasiri kuhusu Ngono?

Nifanyeje Kukabiliana na Hisia za Kukosa Ujasiri kuhusu Ngono?

Nifanyeje Kukabiliana na Hisia za Kukosa Ujasiri kuhusu Ngono? 😊

Karibu kwenye makala h... Read More

Je, kwa nini akina mama wajawazito hawatakiwi kunywa pombe?

Je, kwa nini akina mama wajawazito hawatakiwi kunywa pombe?

Wanawake wajawazito ambao hunywa pombe au kuvuta sigara
wanahatarisha afya na maisha ya mtot... Read More

Sheria kuhusu kufanya punyeto

Sheria kuhusu kufanya punyeto

Punyeto ni kupapasa au kusugua kiungo cha uzazi ili uweze kupata
starehe. Hakuna kosa kwa te... Read More

Vidokezo vya Kuwa na Mawasiliano ya Kuaminika na Msichana

Vidokezo vya Kuwa na Mawasiliano ya Kuaminika na Msichana

Leo kwenye makala hii, tutazungumzia vidokezo vya kuwa na mawasiliano ya kuaminika na msichana. N... Read More

Vidokezo vya Kuchagua Tarehe ya Kuvutia na Msichana

Vidokezo vya Kuchagua Tarehe ya Kuvutia na Msichana

Kuchagua tarehe ya kuvutia na msichana inaweza kuwa changamoto sana, lakini kwa bidii na uwezo wa... Read More

Jinsi ya Kuepuka Kupotoshwa kuhusu Ngono na Mitandao ya Kijamii

Jinsi ya Kuepuka Kupotoshwa kuhusu Ngono na Mitandao ya Kijamii

Jinsi ya Kuepuka Kupotoshwa kuhusu Ngono na Mitandao ya Kijamii πŸ“±πŸ”žπŸ”’

Karibu vijana... Read More

Ugumba wa mwanamke unasababishwa na nini?

Ugumba wa mwanamke unasababishwa na nini?

Ugumba wa mwanamke ni hali ya mwanamke kushindwa kupata mimba. Kama kwa wanaume kuna mambo mengi ... Read More

Watu wafanye nini iwapo wamelazimishwa kufunga ndoa na mtu wasiyemtaka?

Watu wafanye nini iwapo wamelazimishwa kufunga ndoa na mtu wasiyemtaka?

Iwapo mtu amelazimishwa
kuingia katika hali ya ndoa
(kuoa/kuolewa) na msichana/
mv... Read More

Je, kuna vipimo ambavyo vinaweza kugundua hali ya kuwepo kwa ualbino wakati kichanga kikiwa bado tumboni?

Je, kuna vipimo ambavyo vinaweza kugundua hali ya kuwepo kwa ualbino wakati kichanga kikiwa bado tumboni?

Hakuna kipimo rahisi cha kuwezesha kuonyesha kama mama
mjamzito amebeba kinasaba cha ualbino... Read More

Je, pombe inaweza kusababisha uitegemee?

Je, pombe inaweza kusababisha uitegemee?

Ndiyo, Kama nikotini, pombe huweza kukufanya mwenye busara
iwapo utakunywa, na ujiwekee kiwa... Read More

πŸ“– Explore More Articles
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About