Sababu ya tatizo la Tumbo kujaa gesi na jinsi ya kujitibu
Date: April 15, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Tatizo la tumbo kujaa gesi husababishwa na kumeza chakula pamoja na gesi inayotolewa katika vyakula mbalimbali tunavokula ambayo hujaa tumboni na kwenye utumbo mdogo. Hali hii husababisha tumbo kujaa au kuvimba na mtu hutoa gesi hiyo kwa njia ya ushuzi na kubeua.
Nini husababisha.
Tatizo ili mara nyingi husababishwa na huambatana na mambo yafuatayo:
1. Kula vyakula vyenye mafuta mengi ambayo huchelewesha tumbo kufunguka kwa ajili ya usagaji wa chakula.
2. Kunywa vinywaji vyenye Carbonates, cola na kula vyakula vyenye gesi kama maharage, bigiji, vitunguu, kabichi n.k
3. Msongo wa mawazo na hasira.
4. Kula haraka haraka na kula unaongea.
5. Uvutaji wa Sigara
6. Magonjwa na maambukizi katika mfumo wa chakula asa kwenye tumbo na utumbo ambayo huzuia kusagwa na kufyonzwa kwa chakula.
Jinsi ya kujitibu.
ยท Kunywa chai ya tangawizi au karafuu itasaidia kupunguza gesi.
ยท Unaweza kunywa glasi moja ya juisi ya Limao baada ya kula.
ยท Tafuna mbegu za maboga zinasaidia kulainisha mfumo wa chakula
ยท Lalia ubavu wa kushoto na pumua kwa kasi ili kupunguza gesi tumboni.
ยท Kunja miguu na ikalie uku ukinyoosha mikono na kuinamia mbele itasaidia.
ยท kuongeza kasi ya mfumo wa chakula kufanya kazi na kuondoa gesi.
ยท Fanya mazoezi mepesi ya kutembea na kuruka ruka.
ยท Kula na tafuna chakula taratibu na epuka vyakula vyenye gesi na mafuta mengi,.
ยท Nenda hospitali kama tatizo ili linaambatana na kuharisha, kutapika, maumivu makali ya tumbo, kinyesi chenye rangi tofauti au damu na maumivu ya kifua.
Please log in or register to leave a comment or reply.
Related Posts
Unapopita maeneo mengi ya mijini na pembezoni wa miji utakutana na wafanyabiashara wa miwa wanaou...
Read More
Tafadhali soma na uwapelekee wengine.
Dr. Chriss Mosby wa Tanzania amegundua kensa mpya kwa...
Read More
Mapera ni matunda yanayo patikana kwa wingi lakini mara nyingi huwa hayapendelewi sana kutokana n...
Read More
Peasi ni tunda ambalo limekuwa halithaminiwi licha ya kuwa na faida lukuki katika mwili wa binada...
Read More
Kitunguu swaumu hujulikana kama kitu cha kushangaza katika tiba huko mashariki ya mbali, Kitunguu...
Read More
Ni kazi ngumu kidogo kuacha uvutaji wa sigara. Uvutaji ni tishio kwa maisha yetu. Yawezekana hufa...
Read More
Kila mmoja wetu anaweza kuwa na sababu tofauti inayoweza kumsababishia msongo (stress). Sababu ku...
Read More
Kila wakati unashauriwa na watalam wa afya ya kwamba unatakiwa kula tende kwa wingi ili kupata fa...
Read More
Hii ni dawa nzuri ya kutibu shinikizo la chini la damu sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamin...
Read More
Naamini umeshawahi kusikia kuhusu changamoto ya uvimbe kwenye kizazi kwa Wanawake yaani Fibroids....
Read More
Leo nimekuletea matumizi ya mbegu ya parachichi yenyewe yaani ile inayokuwa katikati ya tunda la ...
Read More
Kula lishe bora
Chakula unachokula kina mchango mkubwa katika kutibu tatizo hili. Vyakula...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!