Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
eBooks: Biashara - Mbinu za Ujasiriamali na Biashara Kufanya tofauti - Topic 3 - AckySHINE
Kwa nini watu wanapenda pesa
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:07 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Watu wengi tunapenda sana Pesa lakini hatuko tayari kuzifanyia Pesa kazi nikiwa na maana kutumia njia sahihi kuzipata na tunapozipata hatuna Akili ya kuweza kuwa nazo muda mrefu zisiondoke. Kama tujuavyo katika maisha yetu haya Pesa ndio kila kitu,tunahitaji Pesa ili tuweze kufanya mambo mengi mazuri na makubwa.Kitu kinachotukwamisha hatujui tufanye nini ili tuweze kuzipata hizi Pesa na tunapozipata tunakosea tena cha kuzifanyia ili zisipotee tena au zisiishe.
Updated at: 2024-05-23 16:07:15 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
KILA mtu duniani ana ndoto ingawa haijalishi ni ndoto gani uliyonayo. Ndoto uliyonayo ina thamani kubwa kuliko fedha wala kitu chochote kile. Ndoto uliyonayo ina nguvu kubwa ya kubadilisha maisha yako na kukufikisha sehemu ambayo ulitaka ufike ama zaidi ya pale ulipotarajia kufika.
Ndoto yako inaweza kukupeleka sehemu mbalimbali duniani ukazunguka kufanya mambo yako si kwa sababu una fedha sana, bali ni kwa sababu una ndoto. Ni vyema utambue nguvu ya ndoto uliyonayo ni kubwa kuliko fedha.
Jifunze kupitia mfano huu Ili uishi kwa amani na watu
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:10 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Siku moja nilichukua taxi aina ya UBER nikiwa naelekea uwanja wa Ndege Mwl. Nyerere Dereva huku akiendesha kwa ustaarabu sana mara ghafla pasipo kutegemea gari ya taka ikajitokeza mbele yetu kutokea nje ya barabara. Dereva wa taxi kwa umakini na neema ya Mungu akalikwepa gari hilo na ilikuwa kidogo agonge gari zingine mbele yetu.
USHAURI WANGU ANZA KUAJIRIWA KAMA MUWEKEZAJI TU ILI UJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:03 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kwa lugha nyepesi ni kwamba ukiajiriwa maana yake umeshindwa kujitegemea kwa ujuzi wako (yaani hujui ufanyie nini) hivyo umeona uukabidhi ujuzi wako kwa wenye "akili na uwezo" wa kuupangia matumizi ya huo ujuzi wako.
Ndio maana licha ya kwamba elimu ni yako wewe, maarifa ni yako wewe, vyeti ni vyako wewe; na kazi unafanya wewe; lakini hao waliokuajiri ndio wanakuamulia kiasi gani wakulipe! Si hivyo tu bali pia wanao uhuru wa kukupiga mkwara, kukutishia na hata kukufukuza muda wowote (utakapowakosea, watakapojisikia ama watakapokuchoka)! Nini nakwambia? Kama umeajiriwa, usiridhike wala usibweteke na mshahara pekee kwa 100%, hebu jiongeze aiseee, una uwezo wa kuzalisha zaidi sambamba na mshahara (waliojisikia) kukulipa.
Kuwa na kawaida ya kujiwekea Akiba ni njia na Siri ya kuwa tajiri
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:30 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Watu wengi wanajiuliza, βSiri ya utajiri ni nini?β Je ni mbinu gani zinaweza kumsaidia mtu kupata utajiri? Siri kubwaya utajiri ni kujifunza elimu ya namna ya kutafuta mtaji, kuwekeza kwa busara kwa namna ambayo daima panakuwa naziada na faida.